Wasichana na wanawake nchini Tanzania bado wanakabiliwa na changamoto nyingi miongoni mwazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, elimu duni au kiwango cha chini cha elimu na uzazi wa mapema.

Kutokana na changamoto zinazowahusu wanawake na wasichana, shirika letu ni kuwasaidia wanawake na wasichana hao kuwa wanachama wanaoheshimika na wanaohusika katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jamii.

Maono Yetu

Kila Msichana na Mwanamke anapaswa kuwa na fursa ya kufikia uwezo wake kamili na kushiriki na kuchangia katika nyanja zote za maisha.

Dhamira Yetu

Kuwezesha jamii ya wanawake kwa ulinzi dhidi ya unyanyasaji, kutoa ufadhili wa masomo, na ujuzi utakaowawezesha kujikimu kimaisha.